SHULE YA KIJESHI YA TEHAMA

TAARIFA YA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI WA KUJIUNGA NA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2026/2027

Shule ya Kijeshi ya TEHAMA (SKT) imepewa ithibati kwa namba ya usajili SAT/REG/006 kuendesha kozi zinazosimamiwa na baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa kozi za Astashahada na Stashahada ya Teknologia ya Habari.

Dirisha la udahili kwa mwaka wa masomo 2026/2027 litafunguliwa kuanzia 28 Julai 2026. SKT inapokea maombi kwa waombaji wa kozi ya Astashahada na Stashahada ya Teknolojia ya Habari. Sifa za mwombaji ni ifuatazo:-

a. Astashahada ya Teknolojia ya Habari (Basic Technician certificate in IT - NTA level 4)

Elimu kidato cha nne (CSEE) mwenye ufaulu kwa kupata angalau daraja la ā€œDā€ katika masomo manne (4) au zaidi, bila kujumuisha somo la Dini.

b. Stashahada ya Teknolojia ya Habari (Diploma in IT - NTA level 5-6)

  1. Awe amehudhiria na kufaulu Astashahada ya Teknolojia ya Habari (Basic Technician Certificate in IT – NTA Level 4) au fani nyingine inayohusiana. Au,
  2. Elimu ya kidato cha sita (ACSEE) chenye ufaulu wa angalau principal moja katika mojawapo wa masomo yafuatayo; Hisabati, Fizikia, Kemia au Sayansi ya Kompyuta, na ufaulu wa somo moja kwa kiwango cha Subsidiary pass au sawa na hicho.

Inasisitizwa mwombaji anatakiwa kujaza taarifa sahihi pamoja na kuambatisha kibali cha kusoma kutoka kikosini kwake (Kupitishwa na Kamati tendaji). Maombi yafanyike kupitia mfumo wa udahili wa shule ambao ni www.skt.ac.tz Ikumbukwe maombi ambayo hayatakidhi vigezo na masharti hayatafanyiwa kazi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA UDAHILI
SHULE YA KIJESHI YA TEHAMA (SKT)

Dirisha la udahili linafunguliwa 28 Julai 2026 na tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni 26 Oktoba 2026.