Tafadhali zingatia yafuatayo kabla ya kufanya Malipo kupitia MIXX BY YAS LIPA KWA SIMU
a. KANUNI NA MASHARTI
- Gharama ya kufanya malipo ya udahili ni Tshs 20,000/- na si vinginevyo.
- Tunapokea malipo kutoka mtandao wa MIXX BY YAS kwenda MIXX BY YAS LIPA na si vinginevyo.
- Fedha ya Maombi itakayolipwa ikiwa imezidi au kupungua kiwango tajwa hapo juu haitorudishwa.
- Baada ya kufanya malipo hayo muda mchache sana utapokea ujumbe kupitia namba ya MIXX BY YAS iliyotumika kufanya malipo, ujumbe huo wenye code zenye mfanano na MSICT2311(Verification code) ambazo utazitumia ili kuendelea kufanya maombi ya chuo.
- Unakumbushwa kusoma vigezo na sifa kwa waombaji wa kozi husika kwani fedha haitorudishwa kama itatokea umekosa nafasi.
b. JINSI YA KULIPIA
- Bonyeza *150*01# kupata Menu ya MIXX BY YAS
- Chagua namba 5 Lipa Kwa Simu
- Kisha namba 1 Kwenda MIXX BY YAS
- Ingiza Lipa namba
15091269
- Ingiza kiasi cha kulipa
20,000/=
- Ingiza namba ya siri ya tigopesa kutuma Tsh 20,000/= kwenda MILITARY SCHOOL OF ICT .
IMETOLEWA NA:
OFISI YA UDAHILI
SHULE YA KIJESHI YA TEHAMA (SKT)
Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni tarehe 30 June 2025.