SHULE YA KIJESHI YA TEHAMA

TAARIFA YA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAJILI KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026

Shule ya Kijeshi ya TEHAMA (SKT) imepewa ithibati kwa namba ya usajili SAT/REG/006 kuendesha kozi zinazosimamiwa na baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa kozi za Astashahada na Stashahada ya Teknologia ya Habari.

Baada ya dirisha la udahili kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kufunguliwa na NACTVET kuanzia 28 Mei 2025, SKT inapokea maombi kwa waombaji wa kozi ya Astashahada na Stashahada ya Teknolojia ya Habari. Sifa za mwombaji ni ifuatazo:-

a. Astashahada ya Teknolojia ya Habari (Basic Technician certificate in IT - NTA level 4)

b. Stashahada ya Teknolojia ya Habari (Diploma in IT - NTA level 5-6)

Inasisitiswa ili kufanikisha udahili kwa kozi hizo waombaji wanatakiwa kutuma taarifa zote zinazohitajika kwa usahihi wakiambatisha kibali cha kusoma kutoka kikosini kupitia mfumo wa udahili wa shule ambayo ni www.skt.ac.tz. Ikumbukwe maombi ambayo hayatakidhi vigezo na masharti hayatafanyiwa kazi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA UDAHILI
SHULE YA KIJESHI YA TEHAMA (SKT)

Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni tarehe 30 Jun 2025.